Balozi Seif na Viongozi wengine wa Serikali waenda kuifariji Familia ya aliekuwa katibu mkuu
Na Thabit Hamidu, Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameongoza Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuifariji Familia ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara marehemu Juma ali Juma.
Ujumbe huo ulifika Kijichi katika Makazi yake na kuifariji familia ambapo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali waliongozana na Makamu wa Rais katika kuifariji Familia hiyo kufuatia kifo cha mpendwa wao.
Marehemu huyo alifariki Jana katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipata matibabu baada ya kupata ajali ya gari, Mazishi yake yamefanyika leo katika makaburi ya mwanakwerekwe Mjini Magharib Unguja.
No comments