Mwanafunzi wa kidato cha pili ajinyonga Mwanza
Na James Timber-Mwanza
Mwanafunzi Masumbuko Kaselya (23) aliyekuwa anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Nyakasungwa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza amejinyonga baada ya kufanya mtihani wa majaribio wa kujiandaa na Mtihani wa Taifa.
Mkuu wa shule ya Sekondari Nyakasungwa Erikana Mashimba alisema kuwa siku ya Aprili 30 mwaka huu walikuwa na mitihani ya majaribio ghafla mwanafuzni huyo alitoweka alitoweka na Majira ya saa 11 jioni walipata taarifa ya kukutwa mwanafunzi huyo amejinyonga kwenye juu ya mti.
Aidha Mwalimu alieleza kusikitishwa na kifo cha mwanafunzi huyo kwani alikuwa ni moja kati ya wanafunzi waliokuwa wanaongoza kwa kufanya vizuri shuleni hapo ambapo hadi sasa ameshindwa hata kuelewa ni kitu gani kilichomsibu mpaka akachukuwa maamuzi hayo magumu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bulumba Selestini Kamondo alisema kuwa alipata taarifa kwamba kuna mwanafunzi amejinyongwa kwenye mti ambapo alifika katika eneo hilo lakini alikuta tayari amefariki.
Aidha Mkuu wa Wiilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole aliwataka wazazi kuhakikisha wanafuatilia watoto wao katika masomo na kushirikiana nao kwa kila jambo ili kujua maendeleo yao jambo litakalowaondolea msongo wa mawazo na kujiepusha na maamuzi yasiyofaa.
Kipole alitoa rai kwa wanafunzi kujitika katika elimu kwani ndio mkombozi wao na kuavhana na maamuzi yasiyofaa yanayogharimu wazazi, na kuahaidi kutoa taarifa pindi uchunguzi utakapokamilika ili kubaini chanzo cha kifo chake.
Mmoja ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakasungwa Baraka Boniphace anayesoma kidato cha tatu alisema kuwa kujinyonga kwa mwanafunzi mwenzao kumeleta simanzi kuwa na kuwaweka katika wakati mgumu.
No comments