Follow Me On Instagram


Mwanafunzi wa kidato cha pili aliyejinyonga kuzikwa leo


Na James Timber-Mwanza

Mwanafunzi Masumbuko Kaselya (23) aliyekuwa anasoma  kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Nyakasungwa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kisha kujinyonga kwa kamba ya Neti baada ya kutoka kwenye mtihani wa majaribio wa kujiandaa na Mtihani wa Taifa anatarajia kuzikwa leo nyumbani kwao.

Kaka wa marehemu Patrick Crispin ambaye ndiye msemaji wa familia hiyo amesema kuwa mdogo wake anatarajia kuzikwa leo nyumbani kwao kijiji cha Bukokwa kilichopo wilayani hapo.

Patrick amesema baada ya kuona mwili wa mdogo wake ameukuta na makovu kwenye mikono ambayo yameonekana kama mtu kaungua na moto jambo linampa wasiwasi na kutoamini kama ni mawazo ya mdogo wake kufanya maamuzi hayo magumu.

Naye Baba wa Marehemu Crispin Kapongo amesema kuwa amemwachia Mwenyezi Mungu japo  mwanae ameacha pengo kubwa katika familia kutokana na juhudi zake alizokuwa anazionesha alipokuwa shuleni na nyumbani.

No comments