Rapa Soulja Boy atupwa jela miezi nane
Msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani, Soulja Boy amehukumiwa kifungo cha miezi nane jela na siku 265 za kufanya kazi za jamii kwa kosa la kuvunja masharti ya kipindi cha matazamio.
Akiwa mahakamani Jana, Jaji alimueleza rapa huyo kuwa alikuwa anafikiria kumfunga miaka miwili jela lakini ameshawishiwa na namna alivyoishi kwa siku 40 akiwa nyuma ya nondo hivi karibuni.
Soulja alikuwa anatumikia kipindi cha matazamio pamoja na kufanya kazi za umma kwa kosa la kukutwa na silaha ya moto kinyume cha sheria mwaka 2014.
Jaji ameeleza kuwa imebainika hakufanya kazi za jamii kama alivyoelekezwa na kwamba alishirikiana na baadhi ya watu kughushi vielelezo vinavyoonesha kuwa alikamilisha adhabu hiyo.
No comments