Wasiwasi wazidi kuongezeka Sudan
Watawala wa kijeshi nchini Sudan wamesema leo kwamba wanajeshi sita wa vikosi vya usalama wameuawa wakati wa maandamano, wakati kukiongezeka wasiwasi kuhusu muundo wa baraza jipya la mpito linalowashirikisha wanajeshi na raia.
Waandamanaji waliviimarisha vizuizi nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum baada ya pande mbili zinazoshiriki kwenye mazungumzo kutofautiana hapo jana juu ya idadi ya wajumbe wa kutoka kila upande watakaounda baraza hilo.
Waandamanaji hao wanataka kuwa na wajumbe wengi wa kiraia kwenye baraza hilo litakalokuwa na viti 15 pamoja na wawakilishi 7 wa kijeshi.
Kaimu mkuu wa baraza hilo la kijeshi Mohamed Hamadan Dagolo amesema pamoja na vifo hivyo, waandamanaji hao waliyachoma masoko na kuwanyang'anya watu pesa zao.
Awali Dagolo alisema jeshi liko tayari kuzungumza na upinzani lakini likitaka kusimamishwa kwa machafuko kuanzia hii leo.
No comments