Chama cha Madaktari wa usingizi (SATA) chakabiliwa na upungufu wa wataalamu
Chama cha Madaktari wa usingizi (SATA) kimesema kuwa idadi ya wataalamu bingwa wa fani hiyo ya tiba ya usingizi na kuondoa maumivu (Anesthesia)bado haitoshelezi kutokana na mahitaji ya huduma hiyo nchini.
Hayo yamesemwa na Rais wa chama hicho Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa uzinduzi wa mkutano wa sita unaojadili kuhusu ongezeko la magonjwa ya ajali nchini jijini Dar es Salaam.
“Mpaka sasa kuna wataalamu bingwa 40 lakini mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu wa masomo tunatarajia wengine wanane waliopo masomoni watajiunga nasi na kufikia idadi ya karibu 50, mahitaji angalau kila hospitali ya mkoa na wilaya ikiwa na mtaalamu huyu mmoja tunahitaji wawepo 200 kwa kuanzia,” amesema Dk Ulisubisya.
No comments