Waziri wa ulinzi Uingereza afukuzwa kazi
Waziri wa ulinzi wa Uingereza, Gavin Williamson, amefukuzwa kazi baada ya uchunguzi kuitishwa kutafuta 'mchawi' aliyetoa siri za kikao cha ngazi za juu cha baraza la usalama wa taifa.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Downing Street imesema Waziri Mkuu amepoteza imani na uwezo wa waziri huyo kutumikia serikali na kwamba Penny Mordaunt ameteuliwa kuchukua wadhifa wake.
Uchunguzi ulihusu taarifa kuwa Uingereza inakusudia kuiruhusu kampuni ya Huawei kutoka China kushiriki kwa kiasi kidogo katika ujenzi wa mitandao ya mawasiliano ya kisasa, 5G, nchini Uingereza.
Huawei inakabiliwa na tuhuma kutoka Marekani kuwa inatumiwa na serikali ya China kufanya ujasusi kupitia teknolojia zake, lakini Huawei inakanusha.
No comments