DC ang'aka na waajiri wakorofi “Msiwanyanyase wafanyakazi”
Na Ferdinand Shayo,Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Kimanta ameonya tabia ya baadhi ya Waajiri wakorofi wanaowanyanyasa Wafanyakazi wao na kuwataka Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi kuwabaini mapema na kuwachukulia hatua.
DC Kimanta amesema hayo wakati akihutubia katika Siku ya Wafanyakazi mkoani Arusha akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo amewataka Waajiri kuhakikisha kuwa wanajiepusha na vitendo vya unyanyasaji kwani watachukuliwa hatua kali.
Aidha amewataka Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi kutatua kero za wafanyakazi badala ya kusubiri siku ya wafanyakazi na kutoa kero zao.
Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya Wafanyakazi mkoani Arusha (TUCTA) Lota Laizer ameiomba serikali itoe nyongeza ya mishahara pamoja na ongezeko la asilimia la 1 la kila mwaka kama ilivyo matakwa ya sheria.
Laizer amewataka Wafanyakazi kuwa viongozi wa kisiasa wanatekeleza majukumu yao bila kukiuka sheria za wafanyakazi na kutumia lugha za kuwadhalilisha wafanyakazi.
No comments